TAMBUA SAIZI ZA WAYA NA SEHEMU HUSIKA ZINAPOTUMIKA KATIKA KUFANYA WIRING YAKO

____


_______________________________________ 

kuna size nying za wire ila leo nitaelezea size ya waya na utumiaji wake katika kufanya wiring yako.

    16mm² wire...  huu ni waya mkubwa ambao unatumika kutoka kwenye output ya mita ya tanesco na kuingia katika input ya circuit breaker...

    4mm² wire..... huu pia ni saizi ya waya ambao pia unatumika katika kufanya wiring katika nyumba . huu waya unatumika kutoka katika output ya circuit breaker na kuingia katika input ya isolator.. lakini pia saizi hii ya waya unatumika kutoka katika mcb na kupeleka katika jiko(cooker socket). na pia ni vizur kuutumia wire huu kama earthwire.

    2.5mm² wire... huu pia ni saizi ya waya unaotumika katika kufanya wiring yako.sehemu zinazotakiwa kutumika waya wa saizi hii ni:- switch socket, ac, heater, waterpump, n.k..

    1.5mm² wire....  huu pia ni saizi ya waya ambao unatumika ktk kufanya wiring yako ...huu wire unatumika katika kusambazia katika taa zote na pia hutumika katika feni...

     NI MUHIMU SANA KUFATA KANUNI ZA WIRE YAANI SAIZI YA WAYA NA KAZI YAKE KWA USAHIHI ILI KUEPUSHA OVERLOAD KATIKA SAKITI YAKO..


Post a Comment

Previous Post Next Post