UMUHIMU WA RCD/RCCB KATIKA MFUMO WA UMEME

 




RCD ni kifaa kinachotumika kwenye mfumo wa umeme iwe majumbani au viwandani na kinakuwa na uwezo tofauti tofauti kulingana na mhali kinapotumika.

RCD nyingi zinazopatikana ni 30mA,100mA na 300mA.

Kazi ya RCD ni kumlinda mtumiaji wa umeme dhidi ya indirect electric shock. Kama tunavyojua IEC60364 imeeleza kuwa kwa matumizi ya umeme wa AC unaoanzia 50volts na kuendelea mambo haya yafanyike;

1: mashine na vifaa vyote vya umeme vyenye housing ya bati au chuma ni lazima viunganishwe kwenye waya wa earth.

2: kifungwe kifaa kitakachoweza kuzima umeme endapo itatokea umeme unapita kwenye njia ambayo sio yake kama vile housing ya jiko au housing ya pasi.

Na kifaa hicho kitakachofungwa kiwe na uwezo wa;

A: kujizima chenyewe endapo hitilafu niloitaja hapo juu itatokea(automatically)

B; pia kijizime haraka bila kuchelewa(instantaneously or without delay).

Kifaa ambacho kinasifa hizo mbili hapo juu kinaitwa RESIDUAL CURRENT DEVICE (RCD)ndicho kinachotumika kumlinda mtumiaji wa umeme asipigwe shock na umeme ulopotea njia au unaovuja.

Post a Comment

Previous Post Next Post