FAHAMU UMEME NDIO CHANZO CHA UBUNIFU WA VIFAA VYA ELECTRONS

 


Umeme ni nini?

Umeme ni mtiririko wa electrons,ndani ya conductor(kipitisho mfano waya).

Kuna aina mbili za umeme
1.Umeme wa mkondo geu (Alternating Current) au AC

Ni umeme ambao mtiririko wake wa current unakuwa katika mawimbi ambapo chaji yake inaenda katika hali ya chanya na hasi kwa kubadilishana.

Mawimbi haya huwa yana kasi ya kutokea mara 50 hadi 60 kwa sekunde hasa kwa umeme wa majumbani unaoletwa na Tanesco.

2.Umeme wa mkondo mnyoofu (Direct current) au DC
Ni umeme ambao chaji yake haibadiliki hali,ni umeme ambao haupo katika mawimbi ni umeme mnyoofu umeme huu ni sawa na ule wa beteri.

Mambo yanayo kamilisha umeme.

1.Voltage (msukumo)

2.Current ( mtiririko wa electrons)

3.Kipitisho (waya)


MAANA YA VOLTAGE


Voltage ni msukumo wa chaji ndani ya kipitisho kama vile waya.Msukumo huu ndio husaidia kusafirisha current kutoka sehemu moja moja hadi nyingine.


Voltage hupimwa katika kipimo kinacho itwa VOLTMETER na alama ya voltage ni herufi "V"

Kazi ya voltage ni kusukuma electrons za umeme katika kipitisho(waya)


MAANA YA CURRENT

Current ni mtiririko wa electrons katika kipitisho cha umeme,electrons ndiyo bidhaa yenyewe ambayo huitajika kufanya kazi furani kutegemeana na saketi kusika.Mfano electrons huweza kugeuzwa kuwa joto,baridi,mwanga N.k.


Mtiririko wa electrons unapimwa kipimo kinacho itwa AMPEREMETER na alama ya ampere ni herufi "A".Ampere katika mfumo wa kihesabu huwakilishwa na herufi "I"


MAANA YA KIPITISHO

Ni kitu chochote ambacho kinaweza kuruhusu electrons kupita ndani yake,Mfano wa kipitisho cha umeme ni kopa,chuma,aluminium nakadharika.

Vipitisho hutofautiana kwa uwezo wa kupitisha kiwango cha electrons


Resistance ni ukinzani (kizuizi) cha mtiririko wa electrons ndani ya kipitisho(waya).

Kipimo cha resistance ni OHMS na hupimwa na kifaa kinacho itwa OHMETER herufi inayo tambulisha resistance ni "R"


Kwa kuwa resistance inapimwa katika kipimo cha Ohms hivyo kiwango cha resistance katika sakiti huwakilishwa na alama ya Ohms.



UHUSIANAO ULIOPO KATI YA CURRENT,REISTANCE NA VOLTAGE


Uhusiano uliopo kati ya vitu hivi vitatu ndio unakamilisha tendo flani la umeme lililo kusudiwa.

Mfuo wa umeme unaweza kufananishwa na mfumo wa maji.Kama ilivyo kwa maji ya bomba kwamba hufata muelekeo wa bomba hata umeme pia hufata muelekeo wa waya.


Maji yana msukumo wake unao itwa pressure ambayo husaidia maji kutoka katika sehemu moja hadi nyingine,Hata umeme una msukumo wake unao itwa voltage ambao husukuma electron kutoka sehemu moja hadi nyingine.


Maji ndio husukumwa katika bomba ili yakatoke upande wa pili,katika umeme electrons ndio husukumwa ili zifike point ya pili.


Upana wa bomba ndio husaidia maji yakapita mengi au machache,bomba ikiwa nyembamba maana yake ina ukinzani mkubwa hivyo maji yatapita machache,bomba ikiwa pana maana yake maji pia yatapita mengi kwani ukinzani wake pia utakuwa mdogo.


Hali hii ni sawa na waya wa umeme,hivyo waya wa umeme ukiwa mnene utapitisha kiwango kikubwa cha current kwa sababu ukinzani wake utakuwa mdogo lakini kama waya utakuwa mwembamba utapitisha kiwango kidogo cha current kwani ukinzani wake utakuwa ni mkubwa

Post a Comment

أحدث أقدم